Tafadhali subiri..
x

Sauti | Mwanamke Sokoni

Programu ya Sauti ya Mwanamke Sokoni


Shirika la EfG ni asasi isiyo ya kiserikali ambayo dira yake ni kuona hakuna vikwazo vyovyote vya kijinsia kwa wanawake walio katika sekta isiyo rasmi, na pia kuona wanawake wakiwa mbali na aina zote za unyonyaji na unyanyasaji. Baada ya kuona uwepo wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake wa sekta isiyo rasmi hususan wanawake wafanyabishara katika masoko, shirika liliandaa utafiti mnamo mwaka 2009 uliokuwa na lengo la kupata taarifa sahihi inayoonesha hali halisi ya wanawake wa sekta isiyo rasmi ya masokoni. Utafiti huo ulionesha wanawake wengi wafanyabiashara masokoni hawakuwa na uelewa wa haki zao za kushiriki katika uongozi wa masoko; vilevile utafiti ulionesha kutokushiriki kwa wanawake katika uongozi kulisababisha changamoto nyingi zilizoathiri biashara na hazikuweza kutatuliwa kutokana na sauti zao kutokuwa na nafasi katika vyombo vya maamuzi. Vile vile utafiti ulionesha wanawake hawakuwa wameungana na kuuganisha sauti zao ili ziwe na nguvu na ushawishi katika uongozi wa masoko.
Matokeo ya utafiti yalipendekeza kuwepo na mpango shirikishi wa kuwaleta wanawake pamoja na kuwajengea uwezo ili wajue haki zao hususani haki ya kushiriki kwenye uongozi na maamuzi yanayohusu uendeshaji wa masoko na namna ya kuchukua hatua kutatua changamoto zinazowakabili. Na hapa ndipo wazo la Programu ya Sauti ya Mwanamke Sokoni lilipozaliwa. Programu hii inalenga kuhakikisha sauti ya mwanamke mfanyabiashara inasikika kwa kujenga utawala bora katika masoko wenye kushirikisha jinsia zote na kutoa fursa sawa kwa wanawake na wanaume kwa kutokomeza aina zote za ukatili wa kijinsia. Programu hii ilianza rasmi Oktoba 2011, katika masoko 18 yaliyopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar-es-Salaam na baade kusambaa mikoa mingine tisa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Lindi,Mtwara, Mbeya, Iringa, Lushoto –Tanga, Musoma na Dodoma. Kutokana na uzoefu wa Programu hii ya Sauti ya Mwanamke Sokoni mbinu kuu tatu zilizotumika ni; Kunganisha nguvu, Kuwezesha walengwa, na Kuchukua Hatua.
1. Kuunganisha Nguvu: Programu ilijikita katika kuhakikisha inaunganisha nguvu za wanawake katika masoko ili kuwa na sauti mojayenye nguvu. Utafiti ulibainisha kwamba, matatizo ya mwanamke sokoni hayawezi kutatuliwa kama wanawake hawatakuwa na sauti katika vyombo vya maamuzi. Hata hivyo, ili sauti ya mwanamke iweze kuwa na nguvukatika vyombo vya maamuzi ni vema sauti moja moja zikaunganishwa.Kama waswahili wasemavyo, ‘’umoja ni nguvu utengano ni udhaifu’’. Kwa kuzingatia dhana hii, Programu hii ilibaini kutokuwa na umoja baina ya wanawake sokoni. Hivyo basi, Mradi ulijikita katika kuhakikisha unaunganisha wanawake sokoni ili kuwa na sauti moja na yenye nguvu.
2. Kuwezesha Walengwa: Baada ya kuunganisha nguvu za wanawake katika masoko,Mradi ulijikita katika kuwawezesha wanawake kwa kuwajengea uwezo kwa kutoa mafunzo mbalimbali na kupanua uelewa wao katika mambo mbalimbaliyanayowahusu wanawake wa sekta isiyo rasmi. Utafiti wa EfG ulibaini uwepo wa uelewa mdogo wa maswala ya haki za sheria na binadamu, utawala bora, uendeshaji biashara na uwezo wa kuhoji na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa wanawake sokoni. Ili kutatua matatizo haya, Mradi ulitumia mbinu ya kuwezesha inayojumuisha kujenga uwezo wa wadau kwa kutoa mafunzo ya utambuzi wa sheria za biashara, haki za wanawake, uongozi, kukabiliana na ukatili wa kijinsia, kuendesha na kuendeleza biashara na ujasiriamali; ushawishi na utetezi.
3. Kuchukua Hatua: Baada ya kuuganisha nguvu za wanawake na kuwajengea uwezo na uelewa, wanawake walihamasishwa na kuchukua hatua muhimu.Kuchukua hatua ni pale ambapo wanawake wafanyabiashara sokoni wamepata uelewa na ujasiri wa kuchukua hatua stahiki katika kutokomeza ukatili wa kijinsia, kuinuka kibiashara nakutetea haki zao za msingi. Utafiti ulibaini ushiriki mdogo wa wanawake wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi hususani katika masoko na kuhoji masuala ya msingi katika mazingira yao ya kazi. Hali iliyotokana na uelewa mdogo na kutotambua haki na majukumu yao katika kuhoji masuala muhimu ya kupelekea ustawi wa sekta hiyo. Hivyo Mradi ulihamasisha na kuwezesha wanawake kuchukua hatua kwa kuwajengea uwezo Umoja wa Wanawake kufanya utetezi na ushawishi, kutoa msaada wa kisheria na kuchukua hatua za kisheria kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma na kuzuia ukatili wa kijinsia.

Ofisi za EfG

NHC, Mandela Road
Opp. National Stadium, Plot No. 322 (2nd floor)
P.O. Box 79329,
Dar es Salaam,
Tanzania

Mawasiliano

Simu: 0765-477539 (Mkurugenzi)

Simu: 0763-079531 (Afisa Miradi)

Uongozi

Penina Reveta – Mwenyekiti wa bodi

Jane Magigita – Mkurugenzi wa shirika

Tovuti

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu: www.efg.or.tz

x

Usajili wa wanachama

x

Taarifa za mwanachama



x

Wasiliana nasi

Kama una swali au unahitaji msaada wowote tafadhali wasiliana nasi:


Kwa msaada wa kiufundi:

Kama unahitaji msaada wowote wa kiufundi, tafadhali tupigie: 0765 477539

x

Ingia ndani ya mfumo

Tafadhali ingiza namba yako ya uwanachama na neno lako la siri ili uweze kufurahia huduma zingine zitolewazo ndani ya mfumo wa UMAPIDO.